1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saied apata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu Tunisia

8 Oktoba 2024

Rais Kais Saied wa Tunisia ametangazwa mshindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu na hivyo kumuwezesha kusalia madarakani baada ya wapinzani wake kuenguliwa huku taasisi zikifanyiwa marekebisho ili kumpa mamlaka zaidi.

Tunis - uchaguzi wa rais wa 2024
Rais wa Tunisia na mgombea wa urais, Kais Saied akiungana na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi katika mji mkuu wa Tunisia.Picha: Anis Mili/AP/picture alliance

Tume huru ya uchaguzi katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika imesema Rais Saied amepata asilimia 90.7 ya kura. Saied, mwenye umri wa miaka 66, aliahidi kuilinda Tunisia dhidi ya vitisho kutoka nje na ndani na kusema ataisafisha nchi kuwaondoa mafisadi na wote wanaobuni njama. Wakosoaji wamekuwa na wasiwasi wakisema siasa za nchi hiyo zitahodhiwa na mtu mmoja.