Saka aipeleka Arsenal fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
6 Mei 2026
Matangazo
Arsenal imefuzu kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Champions kwa mara ya pili katika historia yao kwa ushindi wa nyumbani wa 1-0 dhidi ya Atletico Madrid na kuihakikishia ushindi wa jumla wa 2-1 katika nusu fainali jana Jumanne.
Bao la nahodha Bukayo Saka muda mfupi kabla kipindi cha kwanza kukamilika lilithibitisha kuwa muhimu kwa Arsenal kushinda pambano gumu ambapo wenyeji waliweka rekodi ya tisa ya kutofungwa katika mashindano ya msimu huu.
Arsenal watakabiliana na mabingwa watetezi Paris St Germain, ambao waliwatoa katika nusu fainali ya msimu uliopita, au Bayern Munich katika uwanja wa Puskas mjini Budapest mnamo Mei 30.
Fainali pekee ya Arsenal katika Ligi ya Mabingwa ilikuwa mwaka wa 2006 waliposhindwa na Barcelona.