1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sakata la ununuzi wa korosho Tanzania lajadiliwa bungeni

Deo Kaji Makomba7 Februari 2019

Baadhi ya wabunge wanataka kujua kwa nini ununuzi wa zao hilo linafanywa tofauti na agizo la Raisi John Magufuli aliyeagiza linunuliwe kwa bei ya shilingi 3300 ilhali baadhi ya wakulima wamekuwa wakilipwa shilingi 2600.

Sakata hilo la ununuzi wa zao la korosho limeibuliwa bungeni mjini Dodoma na mbunge wa Liwale Zuberi Mohamed.
Sakata hilo la ununuzi wa zao la korosho limeibuliwa bungeni mjini Dodoma na mbunge wa Liwale Zuberi Mohamed. Picha: DW/S. Khamis

Sakata la ununuzi wa zao la korosho nchini Tanzania leo hii limetinga bungeni tena huku baadhi ya wabunge wakihoji kuwa kwanini ununuzi wa zao hilo linafanywa tofauti na agizo la Raisi John Magufuli aliyeagiza linunuliwe kwa bei ya shilingi 3300 tofauti na inavyofanyika hivi sasa ambapo wakulima wa zao hilo katika mikoa ya kusini mwa Tanzania wamekuwa wakilipwa shilingi 2600 huku wengine wakicheleweshewa malipo yao.

Sakata hilo la ununuzi wa zao la korosho limeibuliwa bungeni mjini Dodoma hii leo na mbunge wa Liwale Zuberi Mohamed Kuchauka kupitia chama cha Mapinduzi CCM wakati wa kipindi cha maswali mbalimbali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu, aliyetaka kujua ni kwanini hadi hii leo wakulima wengi hawajapata pesa zao wakati korosho zao zimekwishachukuliwa na serikali halikadhalika wakulima wengine wakilipwa kidogokidogo pesa zao kwa bei ya shilingi 2600.

Picha: Aprainores El Salvador

Mara baada ya kuanza kwa msimu wa ununuzi wa zao la korosho nchini Tanzania unaoendelea hivi sasa, serikali ya Tanzania iliamua kuingia moja kwa moja katika ununuzi wa zao hilo baada ya kuonekana wanunuzi wa zao hilo wamekuwa wakiwapatia bei za chini wakulima ambazo hazikidhi gharama walizotumia katika kilimo licha ya kwamba Naibu Waziri kivuli wa kilimo kupitia kambi ya rasmi ya upinzani bungeni Paschal Haonga anasema kuwa kumekuwa na mwenendo mbaya wa ununuzi wa korosho pamoja na madhara mbalimbali ambayo yamekuwa yakijitokeza.

Akizungumza bungeni wakati akijibu maswali ya papo kwa papo, Waziri mkuu wa Tanzania, Kasim Majaliwa amesema kuwa bei ya ununuzi wa korosho iliyotangazwa na Raisi John Maguli ya shilingi 3300 ni kwa ajili ya korosho ya daraja la kwanza na korosho daraja la pili inanunuliwa kwa asilimia themanini ya bei ya daraja la kwanza kwa mujibu wa sheria ya bodi ya korosho na akaongeza kuwa.

Mwandishi: Deo Kaji Makomba

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW