1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sala ya kwanza ya Ijumaa ya Ramadhani yafanyika Jerusalem

20 Februari 2026

Maelfu ya Waislamu walikusanyika leo chini ya ulinzi mkali katika viwanja vya Msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem kwa ajili ya sala ya Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Thailand Bangkok 2025 |  Eid al-Adha
Sala za sikukuu ya Eid al-Adha nchini Thailand mnamo Juni 7,2025Picha: Teera Noisakran/Sipa USA/picture alliance

Sala hiyo huko Al-Aqsa, yalifanyika kwa mara ya kwanza tangu makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas kuanza kutekelezwa mwezi Oktoba.

Ilikuwa fursa ya kwanza ambapo watu wengi waliondoka Ukingo wa Magharibi na kusali katika eneo hilo la mji mkongwe wa Jerusalem tangu kipindi cha Ramadhani mwaka jana.

Lakini Israel ilidhibiti idadi ya Wapalestina walioruhusiwa kuingia kutoka Ukingo wa Magharibi hadi 10,000 na iliruhusu tu kuingia kwa wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 55 na wanawake wa umri wa zaidi ya miaka 50 pamoja na watoto wa umri wa hadi miaka 12.

Awali iliweka vikwazo sawa na hivyo kutokana na wasiwasi wa kiusalama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW