1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Salva Kiir afanya mkutano wa dharura na maafisa wa usalama

22 Novemba 2024

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amefanya mkutando wa dharura na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama saa kadhaa baada ya risasi kufyatuliwa nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa Shirika la Intelijensia Akol Koor.

Rais wa Sudan Salva Kiir akihudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais wa Kenya William Ruto mjini Nairobi mnamo Septemba 13,2022
Rais wa Sudan- Salva KiirPicha: Brian Inganga/AP Photo/picture alliance

Gazeti la Sudan la Post, limemnukuu afisa mmoja wa usalama akisema mkutano huo umeishughulikia mivutano yote mikubwa na kuwa familia ya mkuu huyo wa zamani wa ujasusi wa Sudan Kusini pamoja na familia yake zimehakikishiwa usalama. Hata hivyo bado hakuna kauli rasmi ya serikali kuhusu mkutano huo.

Rais Salva Kiir amfuta kazi waziri wake wa fedha katikati ya mzozo wa kiuchumi

Alhamisi jioni, milio ya risasi ilisikika kwenye eneo la nyumba ya Koor iliyo katika mji mkuu Juba, hali iliyoibua wasiwasi kuhusu usalama wa taifa hilo changa zaidi duniani. Mkuu huyo wa zamani wa Ujasusi wa Sudan Kusini alifutwa kazi na Rais Kiirmwanzoni mwa mwezi Oktoba na kuwekwa chini ya kifungo cha nyumbani. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW