1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Salvador Illa aapishwa kama kiongozi wa Catalonia

10 Agosti 2024

Mwanasiasa wa chama cha kisoshalisti Salvador Illa ameapishwa kuwa rais mpya wa serikali ya jimbo la Catalonia katika sherehe iliyofanyika katika ikulu ya serikali mjini Barcelona.

Uhispania | Salvador Illa
Kiongozi mpya wa Catalonia Salvador IllaPicha: Emilio Morenatti/AP Photo/picture alliance

Salvador Illa aliye na miaka 61 amesema kando na kuchukua kiapo cha kuingoza serikali hiyo pia anarithi matumaini ya watu wa Catalonia.

Katika hotuba yake, kiongozi huyo wa Catalonia ameonyesha nia ya kuzihudumia taasisi zote na kwa kila mtu kuhisi amewakilishwa  katika kazi yake. 

"Ninachukua jukumu hili kwa shauku na heshima lakini pia kwa unyenyekevu wa mtu anaetaka kutoka leo kuwa mtumishi wa kwanza wa umma wa Catalonia. Nia yake ni kuongoza vizuri na kuwa kiongozi wa kila mmoja. Taasisi hizi ni za kila mmoja wenu na zinapaswa kumhudumia kila mmoja. Nataka kila mtu ahisi amewakilishwa huko, hicho ndicho nnachokipigania. Nia yangu ni kuwaunganisha wote na kuwahudumia," alisema Salvador Illa. 

Bunge la Catalonia kumchagua kiongozi mpya bila Puigdemont

Licha ya chama chake kushinda wingi wa viti katika uchaguzi wa bunge mwezi Mei, ushindi huo haukutosha kuunda serikali na inabidi atafute uungwaji mkono wa vyama vingine kuweza kuunda serikali ya pamoja.

Kuapishwa kwake kunachukuliwa kama mwanzo mpya kwa jimbo hilo ambalo limekuwa likikabiliwa na migogoro kadhaa kwa zaidi ya miaka 10 kufuatia matakwa na harakati zake za kutaka uhuru kutoka kwa Uhispania.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW