1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Samia Suluhu Hassan aapishwa rasmi kuwa rais wa Tanzania

3 Novemba 2025

Samia Suluhu Hassan ameapishwa muda mfupi uliopita huko Dodoma, kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi waOktoba 29 uliokumbwa na vurugu.

Tanzania Dodoma | Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Samia Suluhu Haasan aapishwa rasmi kuwa rais wa Tanzania baada ya kushinda uchaguzi uliokumbwa na utataPicha: Michael Jamson/AFP

Rais Samia ameingia madarakani kuongoza muhula wa pili baada ya kupewa ushindi wa asilimia 98 ya kura na Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC).

Hafla ya kuapishwa kwake imefanyika chini ya ulinzi mkali katika uwanja wa kijeshi mjini Dodoma.

Kiongozi huyo ameapishwa huku upinzani ukiyakataa matokeo yaliyommpa ushindi na kusema mchakato wa uchaguzi haukuwa wa huru na Haki.

Hali bado ni tete nchini humo kufuatia maandamano yaliyozuka muda mfupi baada ya uchaguzi kuanza.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW