1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Samia: Tume ya uchunguzi ya mauaji kuundwa nchini Tanzania

14 Novemba 2025

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo ameliambia bunge kwamba tume ya uchunguzi inaundwa kuchunguza mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi ambao ulimrejesha madarakani.

Tanzania Dodoma 2025 | Hafla ya kuapishwa kwa rais Samia
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu HassanPicha: Tanzania State House

Rais huyo amesema anatambua kuwa vijana wengi waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini hawakujua walichokuwa wakifanya.

Ameongeza kusema kama mama wa taifa anaviagiza vyombo vya sheria na hasa ofisi ya mkurugenzi wa polisi kuangalia kiwango cha makosa yaliofanywa na vijana hao na kwa wale watakaonekana walifuata tu umati lakini hawakuwa na nia ya kufanya uhalifu, wafutiwe makosa yao.

Samia atuma salamu za rambirambi kwa waliopoteza wapendwa wao

Rais Samia ameongeza kuwa amesikitishwa sana na tukio hilo na akatoa salamu za rambirambi kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao.

Kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo, Rais Samia alirejea tena madarakani kwa ushindi wa asilimia 98 ya kura za uchaguzi uliofanywa Oktoba 29.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW