SANAA:Ziara ya Schroeder nchini Yemen
3 Machi 2005Matangazo
Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder ametia saini mikataba mitatu ya kiuchumi nchini Yemen katika ziara yake ya mataifa ya ghuba.
Kansela Schroeder pia alifanya mazungumzo na rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh mjini Sanaa.
Mapema Kansela aliwaalika viongozi wa Bahrain na Qatar kuitembelea Ujerumani ili kuzungumzia juu ya mpango wa kujenga reli itakayounganisha nchi hizo za ghuba.