1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTA CRUZ: Wakimbizi watua pwani za Hispania

18 Julai 2006

Hakuna ishara ya kupunguka ile idadi ya wakimbizi wa Kiafrika wanaoelekea visiwa vya Kanary nchini Hispania.Siku ya Jumatatu,Waafrika 250 katika boti tatu,walitua kwenye pwani za visiwa vya Teneriffa na La Gomera kusini mwa Hispania.Miongoni mwao hakuna hata mmoja aliekuwa na pasipoti.Nchini Italia nako,boti tano zilizopakia zaidi ya wakimbizi 650 zilizuiliwa na walinzi wa pwani karibu na Sicily na Lampedusa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW