1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTA MARIA : Kesi ya ngono na mtoto dhidi ya Michael Jackson yaanza

1 Februari 2005

Kesi ya kuharibu mtoto iliokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu inayomkabili muimbaji nyota wa muziki wa pop Michael Jackson hatimae imeanza rasmi katika mahakama ya Carlifonia nchini Marekani.

Kuanza kwa utaratibu wa kuteuwa majaji wa baraza kumefunguwa rasmi kesi hiyo ya miezi sita ambayo yumkini ikashuhudia kufungwa kwa miaka 20 gerezani kwa muimbaji huyo ikiwa atapatikana na hatia.

Jackson anakabiliwa na mashtaka ya kumharibu mvulana wa miaka 13 mgonjwa wa kansa miaka miwili iliopita kwa kumlewesha pombe na kula njama za kumteka nyara pamoja na kufanya maonevu kwa mvulana huyo na familia yake.

Kabla ya kuanza kwa kesi hiyo Jackson alitowa taarifa katika tovuti yake akisisitiza kwamba hana hatia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW