1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Santa Maria—California:kasheshe katika kesi dhidi ya Michael Jackson

15 Machi 2005

Kizungumkuti kimezuka katika kesi dhidi ya mwanamuziki Michael Jackson.Kijana anaemtuhumu Michael Jackson kumnajisi,amekiri jana,madai yxake hayana msingi.Akihojiwa wakili wa Michael Jackson kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 amekiri,aliwahi kumsimulia mwalimu wake wa shule katika mwaka 2003,hakuna chochote kilichotokea kati yake na Michael Jackson.Shahidi huyo wa upande wa mashtaka alionekana akitapa tapa jana kulinganisha na namna alivyokua wiki iliyopita .Michael Jackson daima amekua akikanusha tuhuma za kumnajisi mtoto yeyote yule .Hatima ya kesi haijulikani itakuaje hivi sasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW