1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO DE CHILE: Wanajeshi wafariki kwa baridi milimani

22 Mei 2005

Idadi ya wanajeshi waliofariki katika msiba mkubwa kabisa wa jeshi nchini Chile wakati wa amani,inazidi kuongezeka.Kiasi ya wanajeshi 433, wengi wao wakiwa vijana ambao ndio kwanza wamejiandikisha jeshini,walipelekwa katika milima ya Andes iliyofunikwa na barafu kufanya mazoezi ya kijeshi licha ya kutabiriwa kutakuwepo hali mbaya ya hewa.Kuna khofu kuwa hadi askari jeshi 45 wamefariki baada ya kugubikwa na barafu.Vifo 23 vimethibitishwa na hali mbaya ya hewa inazuiwa juhudi za kuwaokoa wengine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW