1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANTIAGO : Pinchotet aondolewa kinga ya kutoshtakiwa

7 Julai 2005

Mahkama ya Rufaa nchini Chile imemuondolea dikteta wa zamani Augusto Pinochet kinga ya kutoshtakiwa katika kesi ya haki za binaadamu.

Pinochet hivi sasa anaweza kukabiliwa na mashtaka kuhusiana na kuficha mauaji ya mwaka 1975 ya madarzeni ya wafuasi wa sera za mrengo wa shoto katika kile kilichokuwa kikijulikana kama Oporesheni Columbo.Mawakili wake wanategemea kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

Pinochet mwenye umri wa miaka 89 anashutumiwa kwa kuhusika na ukiukaji kadhaa wa haki za binaadamu na amewahi kushtakiwa rasmi katika kesi kadhaa lakini katu hakuwahi kusimama kizimbani kujibu mashtaka hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW