SAO PAOLO : Mkuu wa Kanisa la Kikatoliki ziarani Brazil
10 Mei 2007Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amewasili Sao Paolo akianza ziara yake ya siku tano nchini Brazil.Hii ni ziara yake ya kwanza katika Latin Amerika,ambako wanaishi takriban nusu ya Wakatoliki wote duniani.Rais Luiz Inacio Lula da Silva alimpokea Papa kwenye uwanja wa ndege wa Sao Paolo.Siku ya Ijumaa,zaidi ya watu milioni moja wanatazamiwa kuhudhuria misaa itakayosomwa nje kwenye uwanja,mjini Sao Paolo.Wakati wa misa hiyo,Papa atamtangaza mtawa wa karne ya 18 Antonio Galvao kuwa ni mtakatifu.Vile vile anatazamia kuhotubia mkutano wa maaskofu wa nchi mbali mbali za Latin Amerika na Caribbean katika mji mtakatifu wa Aparecida.Mbali na suala la umasikini mada kuu ya ziara ya Papa Benedikt wa 16 nchini Brazil ni ile idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo wanaotoka kwenye Kanisa la Kikatoliki.