1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarah Mullally ateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Cantebury

3 Oktoba 2025

Uingereza imemteua Sarah Mullally kuwa Askofu Mkuu mpya wa Cantebury Ijumaa. Kuteuliwa kwake kunamfanya mwanamke wa kwanza kuwa kiongozi wa Kanisa la Anglikana nchini Uingereza katika kipindi cha miaka takriban 500.

Uingereza imemteua Sarah Mullally kuwa Askofu Mkuu mpya wa Cantebury
Askofu Mkuu wa Canterbury Sarah MullallyPicha: Mina Kim/REUTERS

Mullally mwenye miaka 63 anakuwa pia mkuu wa takriban Wafuasi milioni 85 wa madhehebu ya Anglikana japo hana mamlaka makubwa.

Aziba nafasi ya Justin Welby

Mfalme Charles III ndiye  kiongozi wa juu kabisa wa Kanisa hilo la Uingereza nafasi iliyoanzishwa katika karne ya 16 baada ya Mfalme Henry VIII  kujitenga na Kanisa Katoliki. Kanisa hilo halikuwa na kiongozi tangu Novemba mwaka uliopita baada ya Justin Welby kujiuzulu kwa kuficha kashfa ya unyanyasaji kwa watoto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW