1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarah Obama azikwa Kogello, nchini Kenya

30 Machi 2021

Sarah Ogwel Onyango Obama, Bibi yake, aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani Barack Hussein Obama amepumzishwa nyumbani kwake kijijini Kogello jimboni Siaya, Nyanza, Magharibi mwa  Kenya. 

Afrika Kenia Sarah Obama Porträt
Picha: Peter Macdiarmid/Getty Images

Katika mazishi hayo ambayo hayakuhudhuriwa na wakaazi wengi wa sehemu hiyo kutokana na kanuni za serikali kupiga marufuku mikusanyiko mikubwa ya watu, yameendeshwa kwa mujibu wa itikadi za dini ya Kiislamu.

Kwenye mazishi hayo, ujumbe wa salamu za rambirambi za waombolezaji, ukiwemo wa Rais Uhuru Kenyatta uliosomwa na Waziri wa nchi za kigeni Rachael Omamo.

Mama Sarah ameendelea kukumbukwa kama mfanisi mkubwa wa miradi ya maendeleo katika jamii pamoja na kujitolea kwake kuwasaidia wasiojiweza akichangia kwa kiasi kikubwa  katika sekta ya elimu. 

Mama Sarah Obama alikuwa mke wa Babu yake Barack Obama, Jaduong Hussein Onyango Obama ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1870 na kufariki tarehe 29 Novemba mwaka 1975. 

Mama Sarah Obama, alitambulika zaidi duniani baada ya mjukuu wake Barack Obama alichaguliwa kuwa seneta wa jimbo la Illinoise - Marekani, kabla ya kushinda uchaguzi na kuwa Rais wa 44 na Rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo kubwa duniani.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW