SiasaUfaransa
Sarkozy aondoka jela akisubiri rufaa yake kuamuliwa
10 Novemba 2025
Matangazo
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameondoka katika jela na sasa atatumikia kifungo chake cha miaka mitano chini ya uangalizi wa mahakama akiwa nje akisubiri uamuzi wa rufaa aliyokata dhidi ya hukumu aliyopewa.
Hayo ni kulingana na uamuzi uliotolewa Jumatatu na mahakama.
Mnamo Septemba, mahakama ya chini ilimhukumu Sarkozy katika kesi ya jinai iliyomhusisha na madai ya kupokea fedha kinyume cha sheria kutoka kwa rais wa zamani wa Libya dikteta Moamar Gadafi kufadhili kampeni.
Sarkozy mwenye umri wa miaka 70 aliamriwa kujiwasilisha gerezani mnamo Oktoba 21, licha ya mawakili wake kukata rufaa.
Punde alipojisalimisha gerezani, Sarkozy aliomba aachiliwe huru kwa masharti.