Sarkozy kushtakiwa kwa kupokea pesa kutoka Libya
26 Agosti 2023Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy atafikishwa mahakamani kwa madai ya kupokea pesa kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa Libya hayati Moamer Gadhafi na kufadhili moja ya kampeni zake za uchaguzi.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa kuanzia mwezi Januari hadi Aprili mwaka 2025 na inatazamiwa kusikiliza ushahidi kwamba mwanasiasa huyo alipanga njama ya kupokea pesa kutoka kwa kiongozi wa Libya ili kufadhili kinyume cha sheria kampeni zake za uchaguzi wa 2007.Rais wa zamani wa Ufaransa apoteza kesi ya rufaa juu ya ufisadi
Sarkozy mwenye umri wa miaka 68 tayari amehukumiwa mara mbili kwa ufisadi na ushawishi katika kesi tofauti zinazohusisha na jaribio la kumlubuni jaji na ufadhili wa kampeni. Rais huyo wa zamani anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi, ufadhili haramu wa kampeni na njama za kutumia vibaya pesa za umma wa Libya.