Sasa ni awamu ya mtoano kombe la dunia
30 Juni 2018Lakini kocha huyo wa Ufaransa anapaswa pia kutafakari kupata kila kitu kutoka kwa wachezaji wa kikosi chake.
Kuingia kwa Ufaransa katika awamu hiyo kutoka katika awamu ya makundi bila matatizo kwa ushindi mara mbili na sare moja kumekifanya kikosi hicho kupigiwa upatu kuishinda Argentina, ambayo ilitandikwa na Croatia na ilihitaji ushindi wa dakika za mwisho dhidi ya Nigeria kuweza kukata tikiti yake kuingia katika awamu hii ya mtoano.
Pia imejitutumua tu katika kundi hilo ambapo haikuonesha umahiri wake katika awamu hiyo ya makundi, ambapo kikosi chake chenye nyota wengi vijana bado hawajaonesha makucha yao katika medani hii kubwa ya dunia.
Messi, nafasi yake katika kombe la dunia na Argentina kumtegemea sana mshambuliaji huyo wa Barcelona , hata hivyo, kumetamalaki katika maelezo kuelekea pambano hili la Jumamosi , saa 10 jioni saa za Ulaya ya kati, ikiwa ni saa 11 saa za Afrika mashariki katika Kazan Arena.
Katika mkutano wake na waandishi habari , Deschamps aliulizwa mara kadhaa vipi Ufaransa itamzuwia Messi, na alijibu taratibu tu , hadi pale swali la nne kama hilo lilisababisha kutoa hisia za kuchoshwa na swali hilo.
"Mchezaji huyu ni wa hali ya juu kabisa kwa hiyo tunapaswa kuchukua tahadhari," nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na mshindi wa kombe la dunia alisema.
Kumnyima mipira Messi kwa kudhibiti sehemu ya kiungo kutaonekana bila shaka ni mwanzo kwa Deschamps kuchukua tahadhari.
Kumfunika Messi
Croatia ilifanikiwa kumfunika Messi kwa kuwa na Ivan Strinic na Marcelo Brozovica kukaa nyuma ya wachezaji wa kati kina Luka Modric na Ivan Rakitic, na kusaidiana kwa kubadilishana katika kukimbia pamoja na mshambuliaji huyo hatari wa Arngentina.
N'Golo Kante na Blaise Matuidi huenda wakalazimika kufanya kazi hiyo, na Deschamps anaweza kuamua kurejea katika mfumo wa msingi wa 4-2-3-1 ambapo Matuidi atakuwa anashika nafasi ya mshambuliaji wa pembeni upande wa kushoto badala ya nafasi ya kushambulia zaidi kama vile anavyocheza mchezaji mwenzake Messi Osmane Dembele katika Barcelona.
Kuweka msisitizo zaidi kwa Messi , hata hivyo, kunaweza kusababisha hali ngumu kwa ushambuliaji wa Ufaransa ambao umeonekana kuwa mkusanyiko wa vifaa ghali ambavyo bado havijaweza kuwa kitu kimoja.
Deschamps alipoteza fursa kwa vijana wake hao kung'aa kwa kubadilisha kikosi chake kilichotoka sare bila kufungana na Denmark, ambayo ilikata tikiti yake ya awamu ya mtoano lakini haijafanya pakubwa kuleta mchezo wa uelewano katika timu.
Mabadiliko mengine yanaonekana kuja katika mchezo dhidi ya Argentina, ambapo Deschamps huenda akamwacha nje mchezaji chipukizi Kylian Mbappe katika benchi tena ama kumpumzisha Pogba.
Katika mchezo mwengine jioni Cristiano Ronaldo, Luis Suarez na Edinson Cavani , Ureno na Uruguay zinajivunia baadhi ya wafungaji bora kabisa katika soka la dunia kwa sasa, lakini Sochi kunaweza kuwa eneo ambalo mpambano wa kombe la dunia unaweza kuleta mvuto mkubwa leo Jumamosi.
Timu hizo zinapambana katika pambano la pili saa mbili usiku kwa saa za Ulaya ya kati na saa 3 usiku kwa saa za Afrika mashariki.
Nchi hizi mbili ndogo zikiwa na utamaduni wa kusifika wa kandanda zinapambana katika pwani ya bahari nyeusi nchini Urusi zikiwania nafasi katika robo fainali ya kombe la dunia mwaka huu 2018.
Kwa Ronaldo ni kwamba anarejea katika uwanja ule ule ambako alipachika mabao matatu dhidi ya Uhispania mapema katika mashindano haya, lakini mara hii atapambana na ngome ya Uruguay ambayo ni pekee miongoni mwa timu 32 zilizofika Urusi na kuingia katika duru ya mtoano bila kufungwa bao.
Hilo na rekodi ya hivi karibuni ya Ureno iliyohusika katika michezo migumu katika awamu za mtoano na kufikia hadi dakika za mwisho, kumeleta uwezekano wa mpambano wa kukata na shoka wakati kombe la dunia linaelekea katika awamu za mwisho.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe/ rtre
Mhariri: Sylvia Mwehozi