Sasa wajumbe wa mkutano wa Davos wabadili mkakati
26 Januari 2008DAVOS:
Wajumbe, katika mkutano wa kiuchumi unaondelea mjini Davos Uswisi,wamebadili mwelekeo na kumulika uwajibikaji.Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa- Ban Ki Moon na waziri mkuu wa Uingereza -Gordon Brown- wamewatolea changa-moto viongozi wa kibiashara kurejelea azma yao yenye lengo la kupunguza, hadi nusu, umaskini katika nchi zinazoendelela kabla ya mwaka wa 2015.Aidha Brown ameomba kuwepo kwa mageuzi katika mashirika ya kimataifa kama vile Benki Kuu ya Dunia na Umoja wa Mataifa, aliyoyasema kuwa hayana ujuzi wa kutosha kukabiliana na changamoto nyingi za wakati huu.Mapema - Katibu Mkuu -Ban Ki-moon alizilaumu nchi tajiri duniani kwa kushindwa kuzisaidia nchi maskini na hivyo kuomba kuzidisha juhudi katika vita dhidi ya umaskani. Mwana harakati na mwana muziki mashuhuri- Bono pamoja na muasisi wa kampuni ya Microsoft-Bill Gates na vilevile mkuu wa umoja wa Mataifa wameweka katika ajenda ya mkutano wa Davos, ili yajadiliwe, masuala ya kutokomeza ugonjwa wa malaria, kuondoa umaskini pamoja na kubadilika kwa hali ya hewa.