1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia iliwanyonga watu 356 mwaka uliopita

1 Januari 2026

Wachambuzi kwa kiasi kikubwa wamehusiha ongezeko hilo la utekelezaji adhabu ya kifo na mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayotekelezwa na utawala mjini Riyadh.

Kunyongwa
Saudi Arabia iliwanyonga watu 356 mwaka uliopitaPicha: Christoph Hardt/Future Image/IMAGO

Mamlaka ya Saudi Arabia imeweka rekodi mpya kwa kuwanyonga watu 356 katika mwaka wa 2025, taarifa hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP ambapo imeongeza kwamba idadi hiyo inamaanisha nchi hiyo imetekeleza adhabu hiyo kwa kuwanyonga wafungwa wengi zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja.

Wachambuzi kwa kiasi kikubwa wamehusiha ongezeko hilo la utekelezaji adhabu ya kifo na mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayotekelezwa na utawala mjini Riyadh huku ikielezwa kuwa wengi waliokamatwa na kutiwa hatiani waliadhibiwa kunyongwa. 

Ni mwaka wa pili mfulululizo kwa Saudi Arabia kuweka rekodi hiyo ya kuwanyonga watu wengi zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja.  2024 watu 338 walinyongwa nchini humo.

Hata hivyo, Wanaharakati mbalimbali wanakosoa hatua hizo kwa madai kwamba mamlaka nchini Saudia Arabia inadhoofisha taswira ya jamii iliyo wazi na yenye uvumilivu zaidi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW