Saudi Arabia inavyowatishia wakosoaji walioko nje
8 Novemba 2019Madai mapya kwamba Saudi Arabia iliwahi kuwalipa wafanyakazi wa zamani wa Twitter nchini Marekani kuwapeleleza wakosoaji wa taifa hilo yanaonyesha namna mkono mrefu wa Riyadh unavyowanyamazisha wapinzani walioko nje. Lakini hizo ndiyo habari tu za karibuni kuhusu mbinu zinazozidi kuwa za kiasa zinazotumiwa na familia tawala kuwazima na kuwatishia watu inaowaona kama tishio kwa mamlaka ya taasisi ya ufalme.
Madai ya karibuni yanakuja katika wakati nyeti. Kampuni ya mafuta ya taifa Aramco haitaki ukosefu wowote wa utulivu wa kisiasa kuathiri hatua yake ya kujiorodhesha kwenye soko la hisa, huku idadi kadhaa ya wanachama mashuhuri wa familia ya kifalme wamehoji uwezo wa mrithi wa ufalme Mohammed bin Salman kuongoza, kufuatia mashambulizi dhidi ya mitambo mikubwa kabisaa ya mafuta mnamo mwezi Septemba.
Kampeni ya kutoweshwa na vitisho imeonegezeka hivi karibuni, baada ya bin Salman kupandisha na kujiimarisha kimadaraka. Ndani ya Saudi Arabia kwenyewe, shirika la Human Rights Watch limezungumzia wimbi la kamatakamata ya watu wengi tangu Salman alivyoteuliwa mrithi wa ufalme mwaka 2017, licha ya ukosoaji wa kimataifa wa mauaji ya kinyama ya mwanadishi habari Jamal Khashoggi mwishoni mwa 2018, na jaribio la kuhamisha nadhari kwa kulegeza udhibiti kwa wanawake. Lakini nje ya falme, Saudi Arabia imebuni mbinu mpya za kuwafikia wakosoaji wake.
Historia ya utowekaji
Ingawa mauaji ya Kashoggi katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul yalivuta nadhari ya kimataifa, falme hiyo imewatowesha kwa muda mrefu watu wanaokosoa utawala wake wanaoishi nje. Mwaka 1979, mpinzani Nassir al-Sa'id alitoweka mjini Beirut.
Na mwaka 2003, mkosoaji wa utawala Sultan bin Turki bin Abdulaziz - mwanafamilia wa familia ya kifalme - alidaiwa kulishwa madawa mjini Geneva na kupelekwa Riyadh, lakini alifanikiwa kutorokea uhamishoni barani Ulaya. Anaripotiwa kurubuniwa kupanda ndege ya Saudi Arabia tena mwaka 2016, na hajaonekana tangu wakati huo.
Mwanamfalme Turki bin Bandar alichapisha picha za video akitoa wito wa mageuzi kutokea Paris kati ya 2012 na 2015, lakini ametoweka tangu wakati huo, kama ilivyokuwa kwa Saud bin Saif al-Nasar, aliekuwa akiishi Milan na aliripotiwa kuunga mkono miito ya kupinduliwa kwa Mfalme Salman.
Teknolojia ya upelelezi ya Saudia
Kwa kuwa sasa mitandao ya kijamii imerahisisha mijadala, utawala wa Saudi umesogeza operesheni zake kuwatishia na kuwanyamazisha watumiaji mashuhuri kwenye Youtube, Twitter na Facebook, na unatumia program za kisasa za uchunguzi kudukuwa akaunti za wapinzani na kutoa vitisho.
Mwaka uliyopita, ndugu na marafiki wa mwanahakati wa Saudi alieko Canada Omar Abdulaziz walikamatwa katika kile alichokiona kama jaribio la kumlaazimisha kuachana na ukoasoaji wake wa mtandaoni.
Baadae akagundua kuwa simu yake ilidukuliwa kupitia huduma ya Whatsapp na kampuni ya ki Israel inayohusishwa na Saudi Arabia kupitia program ya Pegasus.
Abdulaziz na mkosoaji mwingine alieko mjini London Yahya Assiri wote walikuwa washirika wa Jamal Khashoggi. Assiri na mtashtiti wa Youtube Ghanem Almasasir pia walikuja kugundua kuwa simu zao zilikuwa zinafuatiliwa kupitia teknolojia ya Israel.
Mshauri wa juu wa zamani wa Mohammad bin Salman Saud al-Qahtani akasema hata kupitia ujumbe wa twitter kwamba serikali njia za kuwafichua watumiaji wa twitter wanaotumia majina kapuni.
Maelfu ya akaunti bandia za twitter na Facebook zimetumika pia katika nyakati muhimu ili kubali miajdala ya kisiasa upande wa serikali na kuwanyanya watumaji wengine.
Wakati kampuni zote mbili zimejaribu kusimamisha akaunti zinazopigia debe ajenda ya serikali, watalaamu wanasema hatua hizo hazina uwezekano wa kuathiri kiwango kikubwa cha uenezaji wa taarifa za kupotosha.
Kitisho cha twitter
Juhudi hizo, na madai ya karibuni ya Saudi Arabia kuupenye mtandao wa twitter, zinaonyesha ni kiasi gani cha kitisho utawala huo unaona katika majukwaa ya mitandao ya kijamii.
Kwa theluthi moja ya raia milioni 30 wa taifa hilo wakitumia mtandao wa twitter, mtandao huo ndiyo njia kuu ya mazungumzo ya umma.
Wakati Rahaf Mohammed al-Qunun alipoitoroka familia yake na ku tweet akiomba msaada kutoka uwanja wa ndege wa Bangkok mapema mwaka huu, waombaji wengine wa hifadhi kama Dina Ali Lasloom hawakuwa na bahati sawa.
Wanaharakati wengine wengi wa haki za wanawake ndani ya Saudi Arabia, kama Loujain al-Hathloul, wamefungwa gerezani ili kuwazuwia kujaribu kuondoka.
Vita vya Kisaikolojia
Maati Monjib, mchambuzi wa kisiasa katika chuo kikuu cha Mohammed V mjini Rabat, Morocco, anasema wakati mataifa ya kiimla kwa muda rmefu yamedhibiti vyombo vikuu vya habari, kuwasili kwa mitandao ya kijamii kumeziweka tawala hizo kama ufalme wa Saudi Arabia katika shinikizo kubwa.
"Ilibainika wazi kwa tawala hizo za kiimla kwamba hawaku tena na udhibiti wa maoni ya umma, hasa kwa kuibuka kwa watumiaji wakubwa wa mitandao hii ya kijamii," Monjib aliiambia DW.
Lakini wakati alisema imekuwa muhimu kwa mataifa kama hayo kudhibiti mitandao hii, yameitumia pia kwa faida yao kukusanya taarifa kuhusu wapinzani na kuzitumia dhidi yao ili kudhoofisha uaminifu wao na kuwatenga na mitandao yao ya ufadhili.
Mwanaharakati wa Saudia, Abdulaziz Almoyyad aliiambia DW kuwa wakati ukosefu wa uzoefu wa Mohammad bin Salman umempelekea kushughulikia vibaya kabisaa uhusiano wa nje na ndani, utumiaji wa mitandao ya kijamii umeusaidia utawala kuboresha udhibiti wao wa raia wa Saudi Arabia, na kuuruhusu kuendesha kile alichokiita "vita vya kisaikolojia."
Kwa kujenga wasifu wa kila mmoja ambaye utawala unamuona kama mpinzani, "wanajua namna ya kupambana nao," alisema Almoayyad.
"Hebu fikiria hisia kwamba uko nyumbani kwako, ukiwa na familia yako, ukiwa katika wakati wako wa faragha, unaweza kuhisi uwezekano wa kuwa unaangaliwa na kusikilizwa wakati wote.!"
DW imeiomba wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia kutoa kauli.
chanzo: DW