1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia kutumia nyota wa soka kuna athari za kisiasa?

14 Septemba 2023

Saudi Arabia inakosolewa kwa "kutumia michezo" kuziba rekodi yake ya haki za binadamu, kwa kutumia baadhi ya wachezaji maarufu wa kandanda duniani.

Waziri wa michezo Saudi Arabia Abdulaziz bin Turki al-Faisal akiwa katikati
Waziri wa michezo Saudi Arabia Abdulaziz bin Turki al-Faisal akiwa katikati Picha: Saudi Arabian Ministry of Sports//AA/picture alliance

Saudi Arabia inakosolewa kwa "kutumia michezo" kuziba rekodi yake ya haki za binadamu, kwa kutumia baadhi ya wachezaji maarufu wa kandanda duniani.

Wiki iliyopita, mchezaji wa soka wa Ujerumani Toni Kroos aliwaambia waandishi wa habari kwamba Saudi Arabia inauharibu mchezo wa soka.

Kroos alisema hatokwenda kwenye ligi ya Saudia kwa sababu ya hali ya haki za binadamu.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani hakuwa peke yake katika malalamiko haya.

Wachambuzi wa masuala ya michezo na mashabiki kwa pamoja wamekosoa ukweli kwamba Saudi Arabia imekuwa ikiwashawishibaadhi ya wachezaji maarufu wa kandanda duniani kwenye ligi yake ya ndani kwa mishahara ya kupindukia ya mamilioni ya dola.

Soma pia:Saudi Arabia na Iran zimebadilishana mabalozi miaka saba tangu mahu

Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, Mbrazil Neymar, mshambuliaji Mfaransa Karim Benzema, Sadio Mane wa Senegal na wengine kadhaa wameingia mkataba na timu za ligi ya soka ya Saudia.

Inakadiriwa mikataba yao mbalimbali inaweza kuwa juu ya dola bilioni 1 katika mishahara kwa wachezaji 20 wa kimataifa.

Soka inamatokeo chanya kwa Saudi Arabia?

Kuongezeka kwa uchunguzi wa kimataifa kunajiri wakati wachezaji wa hadhi ya juu wanapoongezeka, pia umakini zaidi juu ya jinsi Saudi Arabia inatawaliwa kifalme, pamoja na rekodi yake mbaya ya haki za binadamu. 

Mashabiki wa soka Saudi ArabiaPicha: Thaier Al-Sudani/REUTERS

Kampeni ya pamoja ya Saudi Arabia kuchukua nafasi kubwa zaidikatika soka la kimataifa ni sehemu ya mpango kabambe wa dira ya mwaka 2030 wa taifa hilo la Ghuba lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Hatua ambayo inalenga kutanua wigo wake katika uwekezaji mbali na mapato ya mafuta, lakini pia katika sekta kama utalii na burudani.

Soma pia:Saudi Arabia yarefusha muda wa kupunguza uzalishaji mafuta

Kupitia kampeni na ufadhili mbalimbali wa kifedha, Saudia pia wamewekeza kiasi kikubwa katika gofu, kriketi, baiskeli, mashindano ya magari, tenisi na mieleka. Hata hivyo, kandanda haikuwa kwenye ajenda kila wakati.

James Dorsey, mtaalam wa soka katika Mashariki ya Kati, amesema kwamba washauri wa kwanza kufanyia kazi mkakati wa kitaifa wa michezo wa Saudi Arabia walitakiwa kuzingatia michezo ya mtu binafsi kama tenisi au gofu badala ya michezo ya timu.

Historia: Matokeo ya siasa katika soka

Kuna mifano mingi ya kihistoria ya jinsi soka inaweza kuleta matatizo ya kisiasa katika eneo hilo.

Mnamo 1958, wakati wa kampeni ya Algeria ya kupata uhuru wake kutoka kwa mkoloni, Ufaransa, baadhi ya wachezaji bora wa Algeria walisababisha utata kwa kujiondoa kutoka kwenye ligi ya soka ya Ufaransa na kuunda timu yao ya taifa, inayojitegemea.

Mnamo mwaka 2000, mashabiki wa soka wa Libya waliuvamia uwanja wa Benghazi baada ya mchezo usio wa haki dhidi ya klabu inayomilikiwa na mtoto wa dikteta Moammar Gadhafi.

Kikosi cha timu ya soka Saudi ArabiaPicha: Kevin Manning/Action Plus/IMAGO

Mwaka 2011, mashabiki wa soka nchini Misri waliojulikana kama "ultras" walichangia pakubwa katika mapinduzi ambayo hatimaye yalimwondoa dikteta wa muda mrefu wa nchi hiyo, Hosni Mubarak.

Soma pia:Tawala za Mashariki ya kati na teknolojia ya akili bandia

Na hivi majuzi, Qatar ilibadilisha sheria zake za kazi baada ya kukosolewa kimataifa kabla na wakati wa Kombe la Dunia la kandanda la 2022, ambalo iliandaa.

Licha ya mifano kama hii, ushauri wa kujiepusha na michezo ya timu unaonekana kufutwa baada ya 2018, wakati Mwanamfalme mashuhuri wa Ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman alipoimarisha umiliki wake wa madaraka.

Baada ya kuangalia kwa undani Kombe la Dunia la 1978 nchini Argentina, Adam Scharpf, mmoja wa waandishi wa utafiti na profesa msaidizi wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Copenhagen, na watafiti wengine walihitimisha kuwa tawala za kiimla zinafahamu vyema hali ya pande mbili za matukio makubwa ya michezo na hupanga mikakati kwa makusudi kukabiliana nayo.

Hizi zinaweza kujumuisha kuongezeka kwa vurugu kabla na baada ya tukio na kuongezeka kwa ufuatiliaji.

Kwa hakika, licha ya matumaini yote kuhusu michezo kuwa kichocheo cha mabadiliko mazuri ya kijamii, soka ni chombo tu, Dorsey alisema.

Iwapo italeta mabadiliko au la inategemea hali na jinsi viongozi wa kisiasa wanavyochagua kuitumia.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW