SiasaSaudi Arabia
Saudi Arabia na Qatar waikosoa miito ya Israel kuhusu Wagaza
4 Januari 2024![Nchi kadhaa zalaami mpango wa Israel wa kuwahamisha wakaazi wa Gaza](https://static.dw.com/image/67873749_800.webp)
Matangazo
Waziri wa Usalama wa Taifa, Itamar Ben-Gvir siku ya Jumatatu alitoa wito wa kuendeleza suluhisho la kuwahimiza wakazi wa Gaza wahame na kuanzishwa tena kwa makazi ya Israeli katika Ukanda wa Gaza, siku moja baada ya Waziri wa Fedha mwenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia, Bezalel Smotrich kutoa matamshi kama hayo.
Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Saudia imesema Saudi Arabia inalaani na kukataa matamshi ya mawaziri hao wawili. Marekani, Ufaransa na Umoja wa Ulaya pia wameshutumu kauli hizo.