Saudi Arabia yaandaa mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine
5 Agosti 2023Mkutano huo unaofanyika leo mjini Jeddah, unashiria utayarifu wa Saudi Arabia wa kutoa mchango wake ili kuleta suluhisho la amani ya kudumu. Urusi haitahudhuria mkutano huo. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameunga mkono kufanyika mkutano huo unaohudhuriwa na wajumbe kutoka nchi mbalimbali ikiwa pamoja na nchi zinazoendelea ambazo zimeathirika na kupanda kwa bei za vyakula kutokana na vita.
Soma zaidi: China kushiriki mazungumzo ya Jeddah kuhusu mpango wa amani wa Ukraine
Zelensky amesema mazungumzo ya mjini Jeddah ni muhimu kwa sababu masuala ya chakula, usalama na hatma ya mamilioni ya watu duniani yanategemea juhudi zitakavyofanyika ili kuutekeleza mpango wa amani. China ambayo imekataa kuilaani Urusi kwa kuivamia Ukraine pia inawakilishwa kwenye mkutano huo wa mjini Jeddah.