SiasaSaudi Arabia
Saudi Arabia yakubali kushirikiana na China
29 Machi 2023Matangazo
Mbali na China, washirika wengine katika muungano huo ni Urusi, India, Pakistan na nchi nne za Asia ya kati ambazo ni Kazakhstan, Kyrgyzstan, Uzbekistan na Tajikistan. Ushirika huo ulindwa mwaka 2001 kama muungano wa kisiasa, kiuchumi na kiusalama dhidi ya taasisi za kimagharibi. Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia, SPA limesema uamuzi wa kujiunga na Muungano wa Ushirikiano wa Beijing ulichukuliwa katika kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Mfalme Salman wa Saudi Arabia. Nchi nyingine zenye hadhi ya mshirika katika mjadala kwenye muungano huo ni Misri, Iran na Qatar.