1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yatishia hatua za kijeshi Yemen

27 Desemba 2025

Saudi Arabia imeonya kuwa iko tayari kuingilia kijeshi na kuiunga mkono serikali ya Yemen endapo mapigano na vikosi vya waasi wanaotaka kujitenga yataendelea.

Yemen Aden 2025 | Wanaotaka kujitenga wakilinda ikulu ya rais baada ya kuchukua mamlaka
Jeshi tiifu la wanaotaka kujitenga wakilinda ikulu ya rais baada ya kuchukua mamlaka.Picha: Fawaz Salman/REUTERS

Onyo hilo limetolewa kufuatia mashambulizi ya anga yanayodaiwa kufanywa na Saudi Arabia katika eneo la Hadramawt, huku Marekani ikitoa wito wa kujizuia na kuendeleza diplomasia.

Vikosi vya wanaotaka kujitenga vinavyoungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu vimepiga hatua kubwa katika wiki za hivi karibuni, jambo ambalo wachambuzi wanasema limeiweka Saudi Arabia katika hali ya kudhalilika.

Mafanikio ya vikosi hivyo yameongeza mvutano kati ya Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, ambazo zinaunga mkono makundi tofauti ndani ya serikali ya Yemen, huku wote wakipinga waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW