Saudi Arabia yatuma mjumbe kwenye ukingo wa Magharibi
26 Septemba 2023Matangazo
Saudi Arabia iliyoingia kwenye mazungumzo na Israel, yanayosimamiwa na Marekani kujaribukurudisha mahusiano ya kidiplomasia, leo imepeleka ujumbe wake katika eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu na Israel.
Soma piaSaudia yasifu "matokeo chanya" ya mazungumzo na waasi wa Houthi wa Yemen
Ujumbe huo unaongozwa nabalozi wake nchini Jordan, ambaye pia anashughulikia Mamlaka ya Wapalestina, Nayef al Sudairi, na anatarajiwa kukutana na Rais Mahmoud Abbas pamoja na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Palestina, Riyad al-Maliki.
Saudi Arabia inasema ziara ya balozi wake huyo inanuwia kufungua njia ya kumaliza mgogoro kati ya Israel na Palestina.