1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudi Arabia yawanyonga watu zaidi ya 100

17 Novemba 2024

Shirika la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Ulaya na Saudi Arabia (ESOHR) limesema Saudi Arabia imewanyonga zaidi ya raia wa kigeni 100 mwaka huu ambapo ni ongezeko kubwa la adhabu ya kunyongwa nchini Saudi Arabia.

Indonesien, Jakarta | adhabu ya kifo Saudi Arabia
Raia nchini Indonesia wakiandamana kupinga adhabu ya kifo nchini Saudi Arabia.Picha: Andrew Lotulung/NurPhoto/picture alliance

Kifo cha karibuni zaidi ni cha siku ya Jumamosi (Novemba 16) katika mkoa wa kusini magharibi wa Najran, ambako raia mmoja wa Yemen aliyepatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya alinyongwa, kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Saudi Arabia lililoripoti juu ya kutekelezwa adhabu hiyo.

Soma zaidi: Mashirika: Adhabu ya kifo Tanzania ifutwe

Mkuu wa shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Berlin, Jeed Basyouni, amesema kwamba idadi ya watu watakaonyongwa inaelekea kuzidi watu 300 mwaka huu na kwamba huu ni mgogoro ambao haujawahi kushuhudiwa nchini Saudi Arabia. 
Wageni walionyongwa mwaka huu ni pamoja na watu 21 kutoka Pakistan, Wayemen 20, watu 14 kutoka Syria, Wanigeria 10, watu tisa kutoka Misri, Wajordan wanane na raia saba kutoka Ethiopia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW