Saudia yamualika Bashir kukutana na Trump
17 Mei 2017Matangazo
Afisa aliyezungumza na shirika la habari la AFP hakusema iwapo Rais al-Bashir atakuwepo katika mkutano wa mwisho wa ngazi ya juu kabisa siku ya Jumapili.
Kuanzia Jumamosi, Rais Trump anatarajiwa kufanya ziara nchini Saudi Arabia ambako kuna sehemu takatifu kabisa za kiislamu, hiyo ikiwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu alipochukua hatamu za uongozi mwezi Januari.
Rais Bashir ameweza kukwepa kukamatwa tangu alipowekewa waranti na Mahakama ya Kimataifa mwaka 2009, kwa tuhuma za mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu vilivyofanywa katika jimbo la Darfur, ambako watu wasiopungua 300,000 wamepoteza maisha.