1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saudia yaonya kutokea janga iwapo Israel itaivamia Rafah

10 Februari 2024

Saudi Arabia imesema operesheni ya jeshi la Israel inayopangwa kuendeshwa mjini Rafah itasababisha "janga la kibinadamu" huku ikilitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Rafah | Israel
Israel yajitayarisha kuendesha operesheni zake mjini RafahPicha: Ibraheem Abu Mustafa/REUTERS

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya ufalme huo, imeeleza wazi kuwa Saudi Arabia inapinga na kulaani vikali hatua hiyo, huku ukionya juu ya kile walichokiita "athari za mashambulizi ya kuvizia" huko Rafah na kitendo cha kuwahamisha kwa mabavu raia wa Palestina. 

Taarifa hiyo ya Saudia imesisitiza kuwa ukiukwaji huu unaondelea wa sheria za kimataifa za kibinadamu, unaonyesha ulazima wa kuitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuizuia Israel kusababisha maafa zaidi ya kibinadamu. 

Israel yapanga kufanya operesheni ya ardhini mjini Rafah

Siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliamuru jeshi lake kujiandaa kuwahamisha raia kutoka Rafah kabla ya operesheni iliyopangwa ya ardhini dhidi ya kundi Hamas katika mji huo wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wanakoishi Wapalestina zaidi ya milioni moja waliokimbia makazi yao.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW