1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SC Paderborn yasajili kipa na mshambuliaji

Deo Kaji Makomba
3 Juni 2020

Taarifa ya kusajiliwa kwa wachezaji hao, imethibitishwa Jumatano na uongozi wa klabu hiyo ambayo hivi sasa inapambana kujiokoa katika mkasi wa kushuka daraja.

Fußball Bundesliga | Borussia Dortmund v SC Paderborn 07 |  Streli Mamba
Wachezaji wa SC Paderborn wakishangilia miongoni mwa mabao katika moja ya mechi ya Bundesliga.Picha: Getty Images/Bongarts/J. Schüler

Klabu ya soka ya Paderborn inayoshiriki ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, imewasajili wachechaji wawili akiwemo mlinda mlango Moritz Schulze pamoja na mshambuliaji Paschal Steinwender ikiwa ni juhudi za kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya misimu miwili ijayo ya ligi hiyo.

Taarifa ya kusajiliwa kwa wachezaji hao, imethibitishwa Jumatano na uongozi wa klabu hiyo ambayo hivi sasa inapambana kujiokoa katika mkasi wa kushuka daraja.

Schulze mwenye umri wa miaka 19 anahamia klabu hiyo ya Paderborn akitokea katika klabu ya RB Leipzig katika kikosi wachezaji walio chini ya umri wa miaka wakati Steinwender anajiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Oldenburg ya daraja la nne.

"Moritz na Paschal ni wachezaji wawili wazuri sana, ambao wanataka kupiga hatua nyingine katika maendeleo yao ya michezo na sisi,"alisema Fabian Wohlgemuth, afisa mkuu mtendaji wa michezo katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa klabu hiyo.

Klabu ya Paderborn kwa hivi sasa inaburura mkia katika msimamo wa ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga ikiwa na alama Nane kibindoni huku ikisaliwa na michezo mitano katika msimu wa ligi hiyo iliyochelewa kumalizika kufuatia mripuko wa virusi vya Corona.

Chanzo/dpa

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW