Schalke kuamua iwapo itamaliza mechi za msimu huu
23 Aprili 2021"Ninaweza kuvumulia iwapo mchezaji hataki kuicheza Schalke katika michezo minne iliyobaki," Mshirikishi wa bodi ya michezo Peter Knaebel aliambia jarida la Ijumaa la Bild. soma zaidi Schalke wamfungisha virago Christian Gross
Knaebel amesema viongozi wanafanya mazungumzo ya kibinafsi na wachezaji na wanawasaidia baada kutukanwa na kushambuliwa na mashabiki baada ya kufungwa na Armenia Belefield 1-0 na kusajili kushuka daraja kwa mara ya 4 katika historia ya klubu ya Schalke 04.
Schalke hawana mechi yoyote wikendi hii baada ya mechi dhidi ya Hertha Berlin kuahirishwa kwa sababu Hertha Berlin ipo katika karantini kutokana na baadhi ya wachezaji kupata maambukizo ya Covid 19.
Mchezo wao unaofuata ni Mei 8 dhidi ya Hoffenheim, na walitarajiwa kuingia mazoezi Jumatano na Alhamisi lakini yamefutwa kufuatia visa hivyo vya mashambulizi. soma Zaidi Schalke yaomba ushirikiano wa mashabiki
Knaebel amesema "wachezaji wako sawa lakini tuna hakika kwamba mazungumzo zaidi yatahitajika. "
Aidha Knaebel amesema kuwa kilabu kitakuwa macho sana katika vipindi vya mazoezi vinavyokuja.
Polisi wa eneo hilo wamesema kuwa Schalke hadi sasa hawajauliza Ulinzi wa polisi, na msemaji akisema wa kituo hicho amesema "tunafanya tathmini ya hatari kwa hali yoyote na tutachukua hatua sisi wenyewe kulingana na matokeo."
Mkuu wa Ligi ya Soka ya Ujerumani (DFL) Christian Seifert amelaani matukio na ametaka hatua kali zaidi zichukuliwe dhidi ya vurugu kama hizo kutoka kwaa mashabiki.
dpa