1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Scholz aahidi mshikamano na Italia juu ya sera ya hifadhi

Daniel Gakuba
8 Juni 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ambaye anafanya ziara nchini Italia leo Alhamis, ameihakikishia nchi hiyo mshikamano katika kupambana na tatizo la waomba hifadhi.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz(kushoto) akisalimiana na waziri mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, alipofanya ziara nchini humo.
Italia inakabiliwa na tatizo la ongezekp la idadi ya wahamiaji na waomba hifadhi, na kuomba ushirikiano zaidi na mataifa mengine ya Ulaya kulidhibiti hilo.Picha: Roberto Monaldo/LaPresse via AP/picture alliance

Kansela Scholz, alipozungumza mjini Berlin kabla ya kuanza ziara yake amesema Italia, Ugiriki na nchi nyingine za kusini mwa Ulaya zinakumbwa na changamoto ya idadi ya wakimbizi inayozidi kuongezeka. Amesema Ujerumani haipaswi kuziacha nchi hizo peke yao, akipendekeza badala yake mshikamano na uwajibikaji kutoka nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Hiyo ni ziara yake ya kwanza Italia tangu Meloni, mwanasiasa wa sera kali za mrengo wa kulia alipoingia madarakani Oktoba mwaka jana. Waziri Mkuu Meloni pia alifanya ziara mjini Berlin mwezi Aprili, na wakati huo Kansela Scholz alibainisha nia ya kuendeleza ushirikiano wa karibu na kiongozi huyo mpya, na kuongeza kuwa makubaliano na serikali ya awali yangeendelea kuzingatiwa bila mabadiliko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW