1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz ampigia simu Zelensky baada ya kuzungumza na Putin

29 Novemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amemuhakikishia rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kuhusu kuendeleza msaada wa kijeshi wa Ujerumani kwa nchi hiyo.

Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Jörg Carstensen/dpa/picture alliance

Haya ni mazungumzo yao rasmi ya kwanza kwa njia ya simu tangu Scholz alipozungumza na rais wa Urusi Vladmir Putin mapema mwezi huu.

Katika ujumbe alioandika katika mtandao wa X, Scholz alisema amekubaliana na Zelenskiy kwamba wataendelea kuwasiliana pia kwa mtazamo wa njia sawa za amani ya haki.

Ukraine: Uamuzi wa Marekani waweza kubadili mwelekeo wa vita

Msemaji mmoja wa serikali ya Ujerumani amesema mazungumzo hayo yalikuwa ya tija na kwamba Zelensky aliishukuru serikali ya Ujerumani kwa msaada wake wa kijeshi hasa katika ulinzi wa anga.

Baada ya mazungumzo ya takriban saa moja kati ya Scholz na Putin mnamo Novemba 15, Rais Zelensky alisema yalizua utata ambao ulidhoofisha juhudi za kumtenga Putin na kumaliza vita ndani Ukraine kwa amani ya haki.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW