Scholz ahimiza mazungumzo juu ya silaha za nyuklia
12 Septemba 2023Akizungumza katika hafla ya kidini mjini Berlin, Scholz ameeleza umuhimu wa udhibiti wa silaha na kuongeza kuwa, tayari nchi kadhaa zimeunda silaha za nyuklia.
Kansela huyo wa Ujerumani amesema silaha za nyuklia ni tishio kwa ubinadamu na ndio maana kuwa wajibu wa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha hazitumiwi
Soma pia:Korea Kaskazini yazindua manowari ya kurusha vichwa vya nyuklia
Ameendelea kueleza kuwa, ni muhimu kuzuia mpango wa Iran wa kurutubisha madini ya Urani ambayo yanaweza kutumiwa kutengeneza silaha za nyuklia.
Kwa mujibu wa taasisi ya kimataifa ya utafiti wa masuala ya amani ya mjini Stockholm SIPRI, idadi yasilaha za nyuklia imeongezekakidogo mwaka 2022 wakati mataifa kadhaa yakielekeza nguvu zao kuimarisha uwezo wao wa kijeshi.