1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz ahimiza ujasiri wa kiraia kuwalinda Wayahudi

Josephat Charo
6 Novemba 2023

Kansela Olaf Scholz amesema "hatutakubali chuki dhidi ya Wayahudi" na yeyote anayewashambulia Wayahudi Ujerumani "anatushambulia sote".

Deutschland Bundeskanzler Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani, Olaf ScholzPicha: Thomas Kienzle/AFP/Getty Images

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewahimiza watu hapa nchini wawalinde wayahudi kufuatia kuripotiwa matukio kadhaa ya chuki dhidi ya wayahudi kuhusiana na mgogoro wa mashariki ya kati. Scholz amesema kuwalinda wayahudi ni suala la ujasiri wa kiraia.

Akizungumza katika mahojiano na gazeti la Mannheimer Morgen yaliyochapishwa hivi leo Scholz amesema yeyeyote anayewashambulia wayahudi nchini Ujerumani anawashambulia watu wote. Scholz aidha amesema chuki dhidi ya wayahudi haitakubalika na Ujerumani ina sheria zilizo wazi kabisa.

Scholz pia amesema ni kosa la uhalifu kuchoma bendera za Israel, kushangilia vifo vya watu wasio na hatia na kupiga kelele za chuki dhidi ya wayahudi. Kauli za kansela Scholz zinakuja kukiwa na wimbi la maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina nchini Ujerumani. Polisi wamepiga marufuku baadhi ya maandamano hayo kwa misingi kwamba yanachochea chuki dhidi ya wayahudi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW