1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aidhinishwa na chama chake kugombea tena Ukansela

25 Novemba 2024

Chama tawala cha Ujerumani cha Social Democrats (SPD) kimemteua Kansela Olaf Scholz kuwa mgombea wake mkuu katika uchaguzi wa mapema utakaofanyika mnamo Februari 23 mwaka ujao.

Kansela Olaf Scholz
Kansela Olaf Scholz.Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Scholz anatarajiwa kuidhinishwa rasmi kwenye mkutano mkuu wa chama cha SPD utakaofanyika Januari 11.

Hayo yameelezwa na vyanzo viwili vya chama hicho cha kisosholisti na hivyo kumpa nafasi Scholz kuongoza kwa muhula wa pili iwapo atashinda kwenye uchaguzi huo. Kura hiyo inafanyika baada ya kuvunjika serikali ya mseto.

Scholz ameteuliwa kuwa mgombea wa chama cha SPD na hivyo kuuzima uvumi wa wiki kadhaa juu ya waziri wa ulinzi Boris Pistorius kujitosa katika kinyang'anyiro hicho cha kugombea Ukansela kwa tiketi ya chama hicho badala ya Olaf Scholz. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW