Scholz aiweka rehani serikali kwa kumtimua waziri wa fedha
7 Novemba 2024Matangazo
Kufutwa kazi kwa Lindner, kutoka chama cha Free Deomcrats (FDP), kilichokuwa mshirika ndani ya serikali ya Scholz kunafungua njia ya kuitishwa uchaguzi wa mapema na kuzusha sekeseke la kisiasa kwenye taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.
Tofauti za kimtamzamo kuhusu namna ya kufadhili bajeti ya taifa zimetajwa kuwa chanzo cha Scholz kumtimua Lindner.
Hivi sasa Scholz atalazimika kuongoza serikali yenye idadi ndogo ya viti bungeni akiwa pamoja na chama kingine mshirika cha Walinzi wa Mazingira, "Die Grüne".
Scholz mwenyewe ametangaza kuuitisha kura ya imani kwa serikali yake mbele ya bunge la taifa Bundestag ifakapo Januari 15 mwaka ujao na iwapo atapoteza kura hiyo uchaguzi wa mapema utaitishwa.