1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Scholz alaani mashambulizi ya Urusi dhidi ya maeneo ya raia

30 Mei 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amelaani mashambulizi ya hivi karibuni ya Urusi yaliolenga makazi ya watu nchini Ukraine.

Estland | Bundeskanzler Scholz in Tallinn
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Ofisi ya Scholz imesema katiaka taafisa kuwa kansela amelaani mashambulizi hayo kupitia mazungumzo ya simu na Rais Volodymyr Zelensky.

Scholz amesisitiza mshikamano na Ukraine wakati ikikabiliana na uvamizi wa shirikisho la Urusi, bila hata hivyo kutaja mashambulizi ya droni yasio kifani yaliofanywa dhidi ya majengo ya makazi mjini Moscow.

Kwa mujibu wa mamlaka ya kijeshi nchini Ukraine mapema leo Urusi imefanya mashambulizi kwa siku ya tatu mfululizo katika mji ya Kiev na kusababuisha kifo cha mtu mmoja.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW