Scholz aliomba bunge kuitisha kura ya imani
11 Desemba 2024Matangazo
Kansela wa ujerumani, Olaf Scholz ameliomba bunge kuitisha kura ya imani wiki ijayo, kufungua njia ya kufanyika uchaguzi wa mapema wa bunge, Februari 23.
Scholz anatarajia kushindwa kwenye kura hiyo ya imani bungeni.
Hatua hiyo rasmi itatowa fursa ya kuvunjwa bunge na kuitishwa uchaguzi katika taifa hilo kubwa kiuchumi barani Ulaya ambalo linakabiliwa na mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.
Kimsingi Kampeini zimekwishaanza zikijikita zaidi kwenye suala la uchumi,vita vya Ukraine na mjadala kuhusu wakimbizi ulioibuka upya kufuatia hali inayoshuhudiwa mashariki ya kati.