1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz apinga wito wa kuongeza bajeti ya ulinzi ya NATO

12 Januari 2025

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameeleza upinzani wake dhidi ya mwito wa Donald Trump kwa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya NATO kuongeza bajeti ya ulinzi hadi asilimia tano ya pato jumla la taifa.

Schoz apinga wito wa kuongeza bajeti ya ulinzi ya NATO hadi asilimia 5 ya pato jumla ya taifa
Schoz apinga wito wa kuongeza bajeti ya ulinzi ya NATO hadi asilimia 5 ya pato jumla ya taifaPicha: Sean Gallup/Getty Images

Scholz ameiambia tovuti ya habari ya Focus Online kwamba kiwango hicho ni kikubwa mno na kuongeza kuwa, upo utaratibu wa wazi ndani ya NATO kuhusu maamuzi kama hayo.

Kansela huyo amesema kwa Ujerumani, nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya, asilimia tano ya pato jumla la taifa ni sawa na takribani euro bilioni 200 kwa mwaka wakati bajeti ya shirikisho la Ujerumani ni euro bilioni 400.

Ameeleza kuwa, ili Ujerumani kutimiza hitaji la Trump, nchi hiyo italazimika kukopa euro bilioni 150 kwa mwaka.

Hata hivyo, amekiri kwamba Ujerumani inapaswa kuwekeza zaidi kwa ajili ya usalama wake, na kusisitiza kwamba Berlin tayari imeongeza karibu mara mbili fedha kwa ajili ya ulinzi kila mwaka hadi karibu euro bilioni 80 katika miaka ya hivi karibuni.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW