1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz ataka waathirika wa Magdeburg wapatiwe msaada zaidi

7 Januari 2025

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani ametaka msaada mkubwa zaidi wa serikali utolewe kwa waathirika wa shambulizi la gari kwenye soko la Krismasi katika mji wa mashariki wa Magdeburg mwezi uliopita.

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani
Kansela Olaf Scholz wa UjerumaniPicha: Soeren Stache/Photoshot/picture alliance

Scholz ameliambia jarida la Stern kwamba anataka waathirika hao wawe na madai bora zaidi ya msaada wa serikali katika kushughulikia matokeo ya mkasa huo.

Kwa sasa, waathirika wa mashambulizi kama hayo wanaweza tu kupatiwa msaada ikiwa tukio limetambuliwa kuwa la kigaidi.

Soma zaidi: Idadi ya waliojeruhiwa katika shambulizi Ujerumani yaongezeka

Katika tukio hilo la tarehe 20 Disemba, mtuhumiwa mwenye uraia wa Saudi Arabia ambaye amekuwa akiishi hapa Ujerumani kwa miaka mingi, aliendesha gari lake kwenye umati uliokuwa wamejumuika katika soko la Krismasi na kuwauwa watu sita na kuwajeruhi wengine 299.

Kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashitaka ya Naumburg, bado wanasaka ushauri wa kitaalamu kuamua endapo mtuhumiwa huyo, aliyetambuliwa kuwa mtu aliyeritadi na mwenye chuki dhidi ya Waislamu, ni mgonjwa wa akili. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW