1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz atoa rai ya utulivu kumaliza mzozo wa kisiasa

9 Novemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa mwito wa kuwepo mjadala wenye tija miongoni mwa makundi ya kisiasa kuhusiana na tarehe ya kuitishwa uchaguzi wa mapema ili kumaliza mzozo wa kisiasa unaoliandama taifa hilo.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Akizungumza na waandishi habari mjini Budapest, Scholz amepuuza madai yanayotolewa na wanasiasa wenzake kwamba anaelenga kuuchelewesha uchaguzi kwa malengo ya kukamilisha kwanza vipaumbele vyake vya kisiasa.

Ujerumani ilitumbukia kwenye mzozo wa kisiasa mapema wiki hii kufuatia kusambaratika kwa serikali ya muungano wa vyama vitatu inayoongozwa na Scholz baada ya kiongozi huyo kumfuta kazi waziri wake wa fedha Christian Lindner.

Uamuzi huo ulimaanisha kwamba serikali ya Scholz imepoteza wingi wa viti bungeni na mwenyewe alipendekeza kuitishwa kura ya imani kwa serikali yake mnamo mwezi Januari na kisha uchaguzi wa mapema hapo mwezi Machi. Hata hivyo chama kikuu cha upinzani cha Christian Democratic Union CDU kinataka uchaguzi ufanyike mwezi Januari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW