1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz atoa wito kwa wakulima kabla ya maandamano

14 Januari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ametoa wito wa kuwa na utulivu wakati ambapo wakulima wenye hasira wakifanya maandamano kwa kuendesha matrekta yao katika mji mkuu, Berlin yalisoababisha msongamano mkubwa.

Wakulima wapanga kuitisha mgomo mkubwa Jumatatu mjini Berlin
Wakulima wapanga kuitisha mgomo mkubwa Jumatatu mjini BerlinPicha: Nadja Wohlleben/REUTERS

Maandamano hayo mapya ni kwa ajili ya kupinga mipango ya serikali inayobatilisha punguzo la kodi ya kilimo.

Scholz katika ujumbe wake amesema ingawa maandamano ambayo ni halali lakini yakigeuka na kuwa ghadhabu au yakipuuza michakato na taasisi za kidemokrasia, basi pande zote zitapoteza.

Maandamano hayo ya wakulima yamesababisha msongamano kutokana na matrekta ya wakulima kuzuia barabara ambapo magari makubwa yanayosafirisha bidhaa katika jiji la Berlin na maeneo mengi ya nchi, yamekwama kwenye misongamano.

Maelfu ya wakulima wanatarajiwa kuhudhuria kilele cha maandamano ya wakulima yatakayofanyika katika mji wa Berlin siku ya Jumatatu. Tukio hilo pia linaungwa mkono na sekta ya usafiri, madereva wa malori na wasambazaji wa mizigo.