1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz atuma risala za rambirambi kwa Iran

21 Mei 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Slcholz leo ametuma risala za rambirambi kwa Iran kufuatia kifo cha rais Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta Jumapili iliyopita.

Kanzler Scholz in Schweden
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Scholz amesema katika ujumbe alioutuma kwa rais wa mpito wa Iran, Mohammad Mokhber, kwamba rambirambi zinakwenda kwa serikali ya Jamuhuri ya kiislamu ya Ian na familia za wale waliokufa katika ajali hiyo.

Raisi, waziri wa mambo ya nje Hossein Amir-Abdollahian na maafisa wengine saba walikufa wakati helikopta walimokuwa wakisafiria ilipoanguka katika eneo la milima kaskazini magharibi mwa Iran karibu na mpaka na Azerbaijan.

Wakati huo huo, maalfu ya Wairan wamejitokeza kuomboleza kifo cha rais wao na kutoa heshima zao za mwisho katika mji wa Tabriz.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW