1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz atumai msaada kuingia Gaza karibuni

Josephat Charo
18 Oktoba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema ana imani msaada huenda ukaruhusiwa kuingia Gaza hivi karibuni kufuatia mazungumzo na viongozi wa Israel, Jordan na Misri.

Kanzler Scholz in Ägypten
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani akiwa ziarani nchini Misri.Picha: Michael Kappeler/dpa/picrture alliance

Scholz ameyasema hao hivi leo wakati wa mkutano na waandishi habari mjini Cairo baada ya kukutana Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri.

Al-Sisi amesema Wamisri wataikataa hatua ya kuwahamishia eneo la Sinai mamilioni ya Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza.

Soma zaidi: Scholz awasili Israel

Kiongozi huyo wa Misri ameongeza kusema kuwa hatua yoyote ya aina hiyo italigeuza eneo la Sinai kuwa kambi ya mashambulizi dhidi ya Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW