1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aunga mkono kufukuzwa wahalifu wa Syria, Afghanistan

6 Juni 2024

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani amesema ataruhusu tena kurejeshwa nchini Afghanistan na Syria kwa watu wanaohusika na uhalifu mkubwa nchini mwake.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Scholz amesema uhalifu na vitisho vya kigaidi havina nafasi nchini Ujerumani. Picha: Political-Moments/IMGAO

Akihutubia bunge la Ujerumani, Bundestag, Alhamisi, Scholz amesema uhalifu na vitisho vya kigaidi havina nafasi nchini Ujerumani. "Lakini pia niweke wazi. Ninakasirishwa wakati mtu ambaye ametafuta hifadhi hapa anafanya uhalifu mkubwa zaidi. Wahalifu kama hao wanapaswa kufukuzwa, hata kama wanatoka Syria na Afghanistan."

Soma pia: Polisi wa Ujerumani wanamshikilia mshukiwa wa tano katika njama ya kanisa kuu la Cologne

Hata hivyo, Scholz hakutoa ufafanuzi kuhusu jinsi hatua hiyo itakavyotekelezwa. Lakini alisema Wizara ya Mambo ya Ndani ilikuwa ikifanyia kazi utekelezaji wake rasmi, na tayari wanaendesha mazungumzo na majirani wa Afghanistan.

Kauli hii ya Kansela Scholz inajiri siku chache baada ya afisa mmoja wa polisi kuuwawa kufuatia shambulio la kisu na raia wa Afghanistan kwenye mji wa kusini magharibi wa Mannheim.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW