Scholz azirai EU na China kujadiliana mvutano kuhusu ushuru
24 Juni 2024Matangazo
Akizungumza katika kongamano la kila mwaka la Shirikisho la Viwanda la Ujerumani, BDI na lenye ushawishi mkubwa, Scholz amesema ni "muhimu" kwa Umoja wa Ulaya na Beijing kufikia maelewano ifikapo mwisho wa mwezi.
Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck, amesema kuna hatari ya kila upande kupoteza kunapokuwa na vita vya biashara vinavyosababishwa na ongezeko la ushuru, baada ya wiki iliyopita kusisitizia umuhimu wa mazungumzo, alipozuru China.
Umoja wa Ulaya ulipanga kupandisha ushuru kutoka asilimia 17.4 hadi 38.1 wa magari hayo kwa muda wa miezi minne, kuanzia Julai 4, hatua iliyochochea mzozo wa kibiashara.